Aina mbalimbali za Visakramenti
Baraka zote -Kanisa linatoa baraka kwa kuliitia jina la Yesu na kwa kufanya ishara ya msalaba. Baraka zote na maombi kwa jina la Yesu Kristo. Kubariki watu, vyakula, vitu na mahali.
Baraka za kudumu za vitu au mahali kwa ajili ya matumizi ya Liturujia - Kutabaruku kanisa -kubariki Makanisa au altare, kubariki mafuta na vyombo vya liturujia na mavazi, na kengele --- au
kuwatoa watu kwa Mungu- mfano abate au abatesa wa monasteri, ibada ya nadhiri za watawa, kuweka wakfu mabikira na wajane, baraka kwa wahudumu fulani, wasomaji, makatekista. . Lile tendo la kuvibariki ni kisakramenti.
Uwingaji -(kupunga nguvu za mwovu) -Kanisa linapotumia mamlaka yake kwa kuliita Jina la Yesu Kristo ili mtu akingwe dhidi ya nguvu ya yule mwovu na kumtoa kutoka utawala wake. Uwingaji wa kawaida (mdogo) hufanyika kabla ya ubatizo. Uwingaji mkubwa hufanywa kwa mamlaka ya Kanisa.
Kuweka nadhiri mikononi mwa mkuu wa Komisarieti
Nadhiri za utawa. Kuwatoa watu kwa Mungu.