KUVISHWA SKAPULARI
KUZIBARIKI
PADRE: Tuombe
Ee Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wa wanadamu, kwa mkono wako wa kuume uzitakatifuze Skapulari hizi ambazo watumishi wako watazivaa kwa uchaji kwa sababu ya upendo wako kwako na kwa Mama Maria wa Mlima Karmeli na walindwe na mitego ya shetani hadi kufa kwao. Tunaomba hayo kwa huyo Kristo Bwana wetu. Amina.
Padre ananyunyiza maji ya baraka
Kuvishwa Skapulari:
Padre: Pokea Skapulari hii takatifu, umwombe Bikira Maria akujalie uivae bila doa la dhambi, akulinde na balaa lolote na akufikishe hadi uzima wa milele. Amina.
Padre: Kwa uwezo niliopewa na Kanisa nakubali ushiriki na wewe katika mema ya kiroho ya shirika la wakarmeli. Amina
Mwisho.
Mungu Mwenyezi, mwumba mbingu na nchi awabariki ninyi aliopenda kuwapokea katika familia ya wakarmeli, awakinge na kitisho cha nyoka wa kale shetani na mtakapokufa awapatie taji ya utukufu pamoja na watakatifu wake wote. Amina.