Mnamo tarehe 10/01/2019 katika Jumuiya yetu ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli MOROGORO tulikuwa na tukio kubwa la kubariki chumba cha sala na kukabidhiwa funguo wa Tarbenakulo. Tukio hilo lilitakiwa kuongozwa na Baba Askofu wa Jimbo la MOROGORO, Mhashamu THERESPHOR RICHARD MKUDE lakini kulingana na sababu isiyoweza kuzuhulika hakuweza kufika kwasababu kulikuwa na tukio la Ushemasi jimboni saa kumi jioni na badala yake Baba Askofu alimtuma Makamu wake padre PATRICK KUNGALO.
Tukio zima lilitanguliwa na adhimisho la Misa Takatifu iliyoanza saa kumi na moja jioni kamili iliyoongozwa na Padre PATRICK KUNGALO (Makamu wa Askofu ) pamoja na mapadre waliofika kwaajili ya kushuhudia tukio zima la kubariki chumba cha sala na kukabidhiwa ufunguo wa Tarbenakulo. Mapadre hao ni wafuatao:
FR.Dominic Maria Somola (O.Carm), FR. Paul Maria Malewa (O.Carm), FR.Victor Maria Biramata (O.Carm), FR.Dominic Wasilewski (O.F.M Conv.), FR.Jerome Munish(O.F.M Conv.), FR.Deodatus Mwagera (P.O.C.R), FR. Emmanuel Chacha (IMC), FR.Genifried Mnai (S.D.S) .
Pia wengine walioudhuria adhimishio Takatifu la Misa ni pamoja na Masista wa USIRINA ndugu zetu wakarmeli wa mabadiliko (O.C.D), Mafrateli toka Shirika la wamisionari wa Adorini, Waseminari wa Shirika la Bikira Maria wa Mlima Karmeli waliopo malezi pamoja na majirani wengine walioalikwa.
Kbla ya utabgulizi wa Misa Takatifu ilisomwa Historia fupi ya Shirika la Bikira Maria wa Mlima wa Karmeli, jinsi lilivyoanzishwa mpaka kufika Tanzania. Katika mahubiri Padre PATRICK KUNGALO alisisitiza wakarmeli kuoshi maisha ya kumfuata Yesu Kristu kama Karama ya Shirika inavyotaka Wakarmeli waishi ili watu wengine waweze kuvutiwa na jinsi wakarmeli wanavyoishi na kumfuata Yesu Kristu ambalo ni lengo letu wote.
Baada ya Komunio Takatifu tuklianza nyimbo za kuabudu na kuandamana taratibu kuingia katika chumba cha sala kwaajili yakuanza kubariki chumba cha sala na kukiabidhiwa funguo ya Tarbenakulo. Zoezi hilo lilifanywa na Padre PATRICK KUNGALO na kusaidiwa na Mapadre waliohudhuria adhimisho la Misa Takatifu na kushuhudiwa na wageni walioalikwa. Baada ya tukio hilo Misa Takatifu iliendelea na kabla ya baraka ya mwisho ya Misa Takatifu, Padre VICTOR MARIA BIRAMATA, (O.carm) mwakilishi wa Mkuu na mlezi alitoa neno la Shukrani kwa wote waliohudhuria Misa Takatifu na kumshukuru FR. PATRICK KUNGALO kwa kukamilisha zoezi zima na kwamba afikishe salamu kwa Baba Askofu kwa kuridhia zoezi zima lifanyike.
Na baada ya hapo Padre Victor M.Biramata alitambulisha wageni waliofika na kushiriki katika tukio zima. Na baada ya Misa Takatifu kulifuatiwa na Tafrija fupi iliyoandaliwa.