Uraia wa Kidijitali

Uraia wa Kidijitali ni nini?

Uraia wa Dijitali unahusisha kuingiliana na wengine mtandaoni kwa njia nzuri na kwa umakini, kutathmini uhalali wa maelezo ya mtandaoni, kutumia teknolojia kwa njia nzuri, kudhibiti muda wa kuwa mtandaoni, kujua jinsi ya kuwa salama mtandaoni, na kutunza vifaa ipasavyo.

Sehemu za Uraia wa Kidijitali

Kudhibiti Muda wa Kutumia Vyombo vya Habari na Athari za Matumizi

Kuelewa jinsi ya kudhibiti muda wa kutumia kifaa katika maisha ya kila siku na kutathmini athari za mwingiliano wa kidijitali kwa ustawi na mahusiano.

Learn More

Faragha na Usalama

Kujifunza jinsi ya kulinda maelezo ya kibinafsi na kukuza uelewa wa kina wa haki za faragha ya data ya kibinafsi ili kujitetea na kuwatetea wengine.

Learn More

Rekodi za Shughuli za Mtandaoni na Utambulisho wa Kidijitali

Kujifunza faida na hasara zinazoweza kutokana na kushiriki maelezo mtandaoni na jinsi wasifu wa kidijitali unavyoweza kuathiri hali ya mtu binafsi, sifa zake na mahusiano yake.

Learn More

Mahusiano na Mawasiliano

Kujifunza kuhusu umuhimu wa kujenga mahusiano chanya, kuepuka mazungumzo yasiyo salama mtandaoni, na kuelewa kwa nini baadhi ya mada na mazungumzo yanapaswa zaidi kuendelezwa mtandaoni au ana kwa ana. 

Learn More

Uonevu kwenye Mtandao, Migogoro ya Mtandaoni, na Matamshi ya Chuki

Kushiriki katika mazungumzo kuhusu mada zinazoibua hisia nyingi na kukabiliana na maingiliano hasi ya mtandaoni ili kukuza jumuiya za mtandaoni zenye maingiliano mazuri na zinazoshirikiana.

Learn More

Uwezo wa Kufikia na Kuelewa Habari

Kutambua vyanzo vinavyoaminika na maelezo ya kuaminika,  huku tukielewa majukumu yetu kama waundaji na watumiaji wa maudhui ya vyombo vya habari.

Learn More

Nyenzo za Wanafunzi

Nyenzo za Walezi