MWEZI JIRANI NA SAYARI TANO ALFAJIRI


MWEZI JIRANI NA SAYARI TANO ALFAJIRI

Katika siku zijazo kuanzia sasa hadi tarehe 7 Februari Mwezi utakuwa jirani na Sayari tanzo tunazoweza kuziona kwa macho moja kwa moja. (Angalia picha ya anga ya alfajiri iliyoambtishwa)

- Mwezi upo jirani na Mustarii (Jupiter) leo usiku hadi alfajiri. 

- Baada ya siku chache, alfajiri ya Februari 1 na 2, Mwezi utakuwa jirani na Mirhi (Mars)

- Februrari 3 na 4 Mwezi utakuwa jirani na Zohali (Saturn)

- Na mwisho, siku za Februrari 6 na 7 alfajiri Mwezi utakuwa jirani na Zuhura na Zebaki ambazo zipo jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza.


Tumia nafasi hii kuweza kutambua Sayari mbali mbali kwa kutumia nafazi zake zitakapokuwa jirani na Mwezi katika siku zijazo wakati wa alfajiri.  Fuata picha iliyambatishwa kurahisisha utambulizi wa Sayari za Musharii (Jupiter), Mirihi (Mars), Zohali (Saturn), Zuhura (Venus) na Zebaki (Mercury). 

 

Mustarii na Zuhura zinan'gaa kuwa uangavu mkali kwa hiyo hutakosa kuzitambua. 

 

Mirihi hun'gaa kwa mwanga mwekundu.   Lakini kuwa macho kuna nyota angavu jirani na Zohali iitwayo Antares, ambayo inang'aa kwa uwekundu kama Mirihi. 

 

Sayari hutaofautiana na nyota za kawaida kwa kutofautiana kun'gaa kwa vile Sayari hun'gaa bila kumeremeta wakati nyota humeremeta.  Kwa hiyo utaweza kutofautisha kati ya Sayari na nyota kawaida.

 

Ukiangalia mandhari hii angani mwenyewe kwa macho yako, utatambua kuwa Sayari zote zimejipanga angani kwa mstari mmoja.  Na hata Mwezi husogea angani kwa kufuata msatari huo. 

 

Hii itawashangaza watu, lakini inaelezeka kwa kuelewa kwamba Sayari zote na Mwezi zipo katika bapa moja nyembaba ambayo huunda Mfumo wa Jua.  Kwa hiyo kwa wakati unaziangalia Sayari na Mwezi kutoka hapa kwetu Duniani, bapa hiyo ya Mfumo wa Jua umejiweka wima anagani na Sayari na Mwezi zipo katika bapa hiyo.

Comments