Mwezi Hilali kusogelea Sayari Zuhura na Sambula angani

Mwezi Hilali kusogelea Sayari Zuhura na Sambula angani

Hali halisi ilivyojionyesha jana Jumatatu, Machi 26 wakati sayari mblili na Mwezi hilali zilipo jipanga kwa mstari ulionyoka na kutoa mandhari ya kusisimua kipekee.

Katika picha, hilali ya Mwezi imebeba sayari ya Zuhura (Venus) inayowaka kama moto angani. Chini yake kushoto katika mstari, ni sayari ya Sambula (Jupiter) ambayo pia inang'aa vikali.

Mpangilio huu hutokea kwa nadra sana kwa vile sayari na Mwezi kila moja huzunguka kwa mpangilio wake wa kasi na umbali. Mkusanyiko kama huu na wa karibu zaidi kuliko huu hautatokea tena hadi Juni 20, mwaka 2015.

Sayari na Mwezi ziko mbali mbali kwa umbali mkubwa sana kati yao. Mwezi upo kilometa kiasi laki nne kutoka kwetu, Zuhura iko kilomita milioni 110, na Sambula iko kilomita milioni 870 kutoka kwetu. Ni kama vile unaziona karibu karibu lakini zimejipanga moja nyuma ya nyingine.

Mandhari za kuvutia sana zitaonekana angani siku za Jumapili na Jumatatu tarehe 25 na 26 Machi, saa moja jioni baada tu ya Jua kuzama chini ya upeo wa Magharibi.

Sayari mbili zinazo n’gaa kwa ukali mkubwa, Zuhura na Sambula zitaungana na Mwezi mchanga hilali ambao utasogea kati ya sayari hizo mbili na kutoa maumbo ya kusisimua. Zuhuara inan’gaa mno wakati Sambula inan’gaa kwa ukali mdodo kidogo.

Picha inaonyesha Mwezi hilali ikiwa chini na kati ya sayari mbili hizo jioni ya siku hizo mbili. Siku inayofuata, Jumanne tarehe 27, Mwezi hilali utakuwa umepanda juu zaidi ya sayari mbili hizo.

Inafaa kukumbuka kwamba katika anga za juu, sayari na Mwezi zinakuwa na umbali mkubwa kati yao kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuja jirani kiasi tunavyoziona kwa macho.