Hazina Iliyosahauliwa hapa Tanzania

Kurasa kuu - Astronomia Tanzania

Hazina Iliyofichika Mbozi, Kusini Tanzania

(English version: The Forgotten Treasure at Mbozi, southern Tanzania)

Masimulizi ya safari yangu, niliyoisubiria kwa hamu kubwa kwa miaka mingi sana, kwenda kuona kimondo kikubwa cha tani 16 cha Mbozi, ambacho kimefichika karibu na Mbeya, kusini mwa Tanzania.

Kimondo hiki ni cha sita kwa ukubwa Duniani, na ni cha pili katika Afrika. Kimondo cha Hobo kilichopo pale Namibia kina uzito wa tani 60 ni cha kwanza kuliko vimondo vyote Duniani.

Kimondo cha Mbozi kipo kiasi cha kilometa 70 kutoka Mbeya, kusini mwa Tanzania, katika njia ya kwenda Tunduma, barabara kuu ya Tanzania-Zambia ambayo inaunda sehemu ya njia kuu ya kuunganisha Afrika kutoka kaskazini Kairo, Misiri, hadi Cape Town, Afrika ya Kusini.

Picha hizi zinaelezea kwa kifupi kuhusu kimondo chetu cha Mbozi. (Haki zote zimehifadhiwa kwa picha zote)

Start from Mbeya

1. Tunaanza safari mji wa Mbeya

2. Kilometa 60 kiasi kutoka Mbeya, katika njia ya kwenda Tunduma na Zambia, tunakata kushoto njia panda ya kwanza mara tu baada ya kijiji cha Mahenje. Barabara nzuri sana, ya udongo, inaelekea eneo la kimondo.

3. Kiasi cha kilometa 10 kutoka njia panda kutoka barara kuu, utakuta njia panda ambapo kuna ubao mdogo tu uliondikwa kwa mkono, neno "Meteorite" na uliowekwa juu kwenye tawi la mti,

4. Mandhari ya enelo la jirani na barabara ya kuelekea kwenye kimondo.

5. Uzio katika njia ya kuingilia kwenye eneo la kimondo.

6. Mkuu wa Kituo cha Kimondo, Nd. Basange, wa Idara ya Kale katika Wizara ya Maliasili na Utalii akiandika hati ya malipo ya kuinigia kwenye eneo la kimondo - shillingi 1,000/= kwa kila mtu.

6. Nilvyoona kimodo kwa mbali kwa mara ya kwanza.

7. Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya Ihanda wakitembelea kimondo kufanya utafiti katika somo lao la Historia katika mwaka wao wa mwisho.

8. Mkuu wa Kituo, Nd. Basange, akitoa maelezo ya awali kuhusu historia na maelezo mengine kuhusu kimondo cha Mbozi.

9. Maelezo ya ziada kutoka kwa Nd. Basange.

10. Muda wangu wa kupiga picha karibu na kimondo cha Mbozi.

11. Picha kutoka upande mwingine wa kimondo. Nyuma yangu ni ukuta uliotokana kuchimbua kimodo chote cha tani 16 kilichokuwa kimefukiwa kabisa zamani.

12. Picha ya upande wa kawaida ya kimondo cha Mbozi.

13. Mwanafunzi David wa Shule ya Sekondari ya Ihanda anayefanya utafiti wa historia ya kimondo.

14. Mwanafunzi Ipyana wa Shule ya Sekondari ya Ihanda.

15. Wanafunzi wakijadiliana maelezo ya kimondo baada ya kuwasikiliza watalamu.

16. Wanafunzi wakijiandaa kurudi shuleni.

17. Kimondo kinawavutia sana wanafunzi kuwa na hamu ya kupiga picha za mwisho.

18. Picha za mwisho na wanfunzi wa Shule ya Sekondari ya Ihanda.

19. Kimondo kinavyoonekana kutoka dirisha la Jumba la Mapokezi. Nyuma ya kimondo unaweza kuona vizuri sana ukuta wa sehemu iliyochimbwa kufufua kimondo.

20. Picha nyingine kutoka dirisha zima la Jumba la Mapokezi.

21. Kimonodo kinavyoonekana kwa upande wa urefu wake.

21. Kimonodo kinavyoonekana upande wa upana wake.

22. Upande wa pili wa kimondo kwa upana wake.

23. Kimondo kinavyoonekana kutoka wa juu ya sehemu iliyochimbwa kufufua kimondo.

24. Picha ya kimondo upande wa urefu wake, ikionyesha sura tofauti kabisa. Kila upande unokiangalia kimondo unaona sura tofauti kwa vile chuma cha kimondo imeyeyushwa sehemu tofauti tofauti na moto wa msuguano na hewa kilivokuwa kinaanguka kutoka angani.

25. Mandhari ya eneo la kimondo inayoonyesha Jumba la Mapokezi pamoja na sehemu ya kuingilia magari. Utaweza kuelewa ukubwa halisi wa kimondo.

26. Kimondo kinachukua sura kama ya gari katika picha hii ya mandhari ya eneo lililochimbuliwa kwa ajili ya kufufua kimondo.

27. Madhari nyingine ya eneo la kimondo kinachoonekana kama vile ni gari.

28. Tunarudi tena njia panda ya Barabara ya Tunduma. Hakuna hata ubao wa kuonyesha hazina kubwa iliyojificha kilometa kumi tu ndani !!

29. Mwenzangu Gabriel akitafuta bila mafanikio, nishani yoyote upande wa pili wa bango la Shule ya Sekondari ya Malangali. Kimondo kinaendelea kufichika........

Kuna umuhimu wa kuvuta Watanzania, na watalii kutoka Duniani kote wanaokuja kuangalia mbuga za kusini mwa Tanzania, waweze kwenda kuangalia hazina yetu kubwa ya tani 16 iliyoanguka katika eneo la Mbozi, miaka zaidi ya1,000 iliyopita na kuchimbuliwa miaka ya 1930.

TANGAZA DUNIANI KOTE

KIMONDO CHETU CHA MBOZI

KINACHOKAA BILA KULALAMIKA

KATIKA KONA YA KUSINI MWA TANZANIA

(English version: The Forgotten Treasure at Mbozi, southern Tanzania)

(Haki za picha zote zimehifadhiwa)

Aprili 2012

Rudi Kurasa kuu wa Astronomia Tanzania