Kitabu cha Mwongozo wa Mwezeshaji Jamii (CBT)
MWONGOZO WA MWEZESHAJI WA JAMII (COPO CBT HANDBOOK)
TOLEO LA KWANZA
JUNI 2026
IMETOLEWA NA:
Community Plus Organization (COPO)
Morogoro, Tanzania
🌐 Website: https://tinyurl.com/copoafrica
📧 Email: copplusorg@gmail.com
HAKI MILIKI (COPYRIGHT)
© 2026 Community Plus Organization (COPO).
Haki zote zimehifadhiwa.
Hairuhusiwi kunakili, kusambaza, au kuchapisha sehemu yoyote ya waraka huu bila idhini rasmi ya Community Plus Organization (COPO).
DIBAJI
Ninayo furaha kuwasilisha Mwongozo wa Community Based Trainers (CBTs)/Wawezeshaji wa Jamii wa Community Plus Organization (COPO), ambao ni chombo rasmi kinachoongoza uteuzi, mafunzo, uthibitishaji na usimamizi wa CBTs katika ngazi zote za utekelezaji.
CBTs ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya jamii, hususani katika kupunguza umaskini uliokithiri, uwezeshaji wa kiuchumi, usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu. Kupitia mfumo huu, COPO inalenga kuifikia jamii moja kwa moja kwa ufanisi zaidi na ushirikiano wa karibu na wananchi.
Mwongozo huu unaweka viwango, taratibu na maadili ya kitaasisi yatakayohakikisha uwajibikaji, uwazi na ubora wa huduma zinazotolewa na CBTs katika ngazi ya kijiji/kata, wilaya na mkoa chini ya usimamizi wa COPO.
Ninawasihi CBTs, viongozi na wadau wote kuusoma, kuuelewa na kuutekeleza kwa umakini ili kufanikishamalengo ya COPO ya kujenga jamii imara, yenye uwezo na inayojitegemea.
Kwa niaba ya COPO, nawashukuru wadau wote wanaoendelea kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo ya jamii.
L ughano Keneth Mwamboghela
Mkurugenzi Mtendaji
Community Plus Organization (COPO)
Juni 2026
SHUKRANI
Community Plus Organization (COPO) inatoa shukrani za dhati kwa wadau wote, viongozi wa jamii, wataalamu na wanachama wanaochangia katika maendeleo ya programu za ukuaji wa Shirika letu.
Shukrani maalum ziwaendee viongozi wa serikali za mitaa, wilaya na mikoa kwa ushirikiano wao katika kuwezesha shughuli za maendeleo ya jamii kwa kulitumia shirika kama mwavuli.
VIFUPISHO
COPO – Community Plus Organization
CBT – Community Based Trainer
CoDO – Community District Officer
CoRO – Community Regional Officer
CDSC – Community Development Support Committee
SDGs – Sustainable Development Goals
M&E – Monitoring and Evaluation
VICOBA – Village Community Bank
NGO – Non-Governmental Organization
HQ – Makao Makuu ya COPO
MWANZO WA MWONGOZO (SDG ALIGNMENT)
Mwongozo huu unaunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs):
SDG 1 – Kutokomeza Umaskini
SDG 5 – Usawa wa Kijinsia
SDG 8 – Ajira na Uchumi Endelevu
UTANGULIZI WA JUMLA (EXECUTIVE OVERVIEW)
“COPO CBT Handbook” ni mwongozo rasmi unaoeleza jinsi Community-Based Trainers (CBTs) wanavyochaguliwa, kufundishwa, kuthibitishwa na kusimamiwa.
CBT ni mtu wa jamii anayesaidia Shirika kufika moja kwa moja kwa wananchi kupitia:
Uhamasishaji wa jamii
Usajili wa wanachama
Mafunzo ya vikundi
Ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo
Ukusanyaji wa taarifa za jamii
CBT ni kiungo muhimu kati ya Shirika na jamii.
MFUMO WA UONGOZI
Mfumo wa uongozi ni wa ngazi 4:
👉 CBT → CoDO → CoRO → COPO Headquarters (HQ)
Maelezo:
CBT – Hufanya kazi moja kwa moja na jamii
CoDO (Community District Officer)
Husimamia CBT kata zote ndani ya wilaya/Halmashauri husika.
CoRO (Community Regional Officer) Husimamia
wilaya/Halmashauri zote ndani ya mkoa
HQ (Makao Makuu) Huongoza sera, uthibitisho na maamuzi ya mwisho
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI
1.1 COPO ni nini?
“Community Plus Organization” (COPO) ni shirika lisilo la kiserikali linalolenga kuboresha maisha ya wananchi kupitia:
Kupunguza umaskini uliokithiri
Kukuza ujasiriamali
Elimu ya jamii
Usawa wa kijinsia
Uwezeshaji wa kiuchumi
1.2 DIRA YA COPO
Jamii yenye uwezo wa kujitegemea kiuchumi na kijamii.
1.3 DHIMA YA COPO
Kuwawezesha wananchi kupitia elimu, ujuzi na miradi ya maendeleo endelevu.
1.4 MAADILI YA COPO
COPO inaongozwa na:
Uadilifu
Uwajibikaji
Uwazi
Ushirikiano
Heshima
Ubunifu
Usawa
1.5 LENGO LA MWONGOZO
Mwongozo huu unalenga:
Kuweka mfumo rasmi wa CBT
Kueleza majukumu ya CBT
Kuweka viwango vya maadili
Kuwezesha uwajibikaji
Kuimarisha utendaji wa jamii
SURA YA PILI: MFUMO WA CBT
CBT anafanya kazi katika mfumo ufuatao:
👉 CBT → CoDO → CoRO → HQ
Majukumu kwa ngazi:
CBT
Kuhamasisha jamii
Kusajili wanachama
Kuendesha mikutano ya vikundi
Kukusanya taarifa
NB: Atakuwa mwenyekiti wa kamati ya wajumbe 5. Afisa Maendeleo Kata ni mshauri wa kamati.
CoDO
Kusimamia CBT wote ndani ya wilaya/Halmashauri
Kuhakikisha taarifa zinawasilishwa kwa wakati
Kuratibu mafunzo
NB: Atakuwa mwenyekiti wa kamati ya wajumbe 5.
Aina ya kiongozi mshauri, itategemea agenda iliyopo
mezani wakati husika.
CoRO
Kusimamia Halmashauri zote ndani ya Mkoa husika
Kuandaa ripoti za mkoa
Kutoa ushauri kwa HQ
NB: Atakuwa mwenyekiti wa kamati ya wajumbe 5.
Aina ya kiongozi mshauri, itategemea agenda iliyopo
mezani wakati husika.
HQ
Uthibitisho wa CBT
Sera na maamuzi ya mwisho
Usimamizi wa kitaifa
SURA YA TATU: SIFA ZA KUWA CBT
Mtu anayestahili kuwa CBT lazima awe na:
3.1 Sifa za msingi
Raia wa Tanzania
Mkazi wa eneo husika
Umri wa miaka 18 au zaidi
Anaweza kusoma na kuandika Kiswahili
3.2 Sifa za tabia
Mtu mwaminifu
Mwenye nidhamu
Asiyekuwa na historia ya rushwa
Anayeheshimu jamii
3.3 Sifa za ziada
Anaweza kuhamasisha watu
Anaweza kuandika taarifa
Ana uelewa wa shughuli za jamii
SURA YA NNE: UTEUZI WA CBT
Mchakato wa uteuzi:
Hatua:
Tangazo la nafasi
Kupokea maombi
Uchambuzi (CoDO)
Usaili
Uteuzi wa majaribio (miezi 3–6)
Tathmini
Uthibitisho na HQ
SURA YA TANO: MAFUNZO YA CBT
CBT hupitia mafunzo haya:
5.1 Mafunzo ya awali
Utambulisho wa COPO
Majukumu ya CBT
Maadili ya kazi
5.2 Mafunzo ya vitendo
Kazi za jamii
Uhamasishaji
Usajili wa wanachama
5.3 Mafunzo endelevu
Mafunzo ya mara kwa mara
Uboreshaji wa ujuzi
Wakati wa mradi maalum
SURA YA SITA: UTHIBITISHO WA CBT
CBT anathibitishwa baada ya:
Kumaliza mafunzo
Kufanya kazi kwa miezi 3–6
Kupata tathmini nzuri
Ngazi:
CBT wa majaribio
CBT aliyethibitishwa
CBT mwandamizi
SURA YA SABA: HAKI NA WAJIBU
Haki za CBT
Kupata mafunzo
Kupata mwongozo
Kuheshimiwa
Wajibu
Kutoa taarifa sahihi
Kuhamasisha jamii
Kufanya kazi kwa uaminifu
SURA YA NANE: TAARIFA NA TATHMINI (M&E)
CBT anatakiwa:
Kutoa ripoti za kila wiki/mwezi
Kuhakikisha taarifa ni sahihi
Kushirikiana na CoDO
Mfumo:
CBT → CoDO → CoRO → HQ
SURA YA TISA: MOTISHA
CBT anaweza kupata:
Vyeti vya pongezi
Mafunzo
Posho (kulingana na mradi)
Tuzo za utendaji bora
SURA YA KUMI: NIDHAMU
Makosa yamegawanyika:
Madogo
Kuchelewesha taarifa
Kati
Kushindwa kufuata maelekezo
Makubwa
Rushwa
Udanganyifu na Uzembe
Hatua:
Onyo
Kusimamishwa
Kuondolewa
VIAMBATISHO
Fomu ya maombi ya CBT (kwenye mfumo)
Kanuni za maadili
Fomu ya ripoti
Tathmini ya CBT
Ahadi ya CBT
MWISHO
COPO inawakaribisha CBT wote kushiriki kikamilifu katika safari hii ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Tunawashukuru kwa kujitoa kwenu, na tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuinua maisha ya wananchi.
Endeleeni kuwa waaminifu, wenye bidii na mfano bora katika jamii. Kumbukeni kuwa kila hatua mnayochukua ni sehemu ya kujenga taifa imara na jamii yenye matumaini mapya.
“Pamoja tunaweza. Endelea kuwa mwanga wa mabadiliko”.
UKURASA WA NYUMA (BACK COVER)
COMMUNITY PLUS ORGANIZATION (COPO)
CBT (Community-Based Trainers) ni mfumo wa wawezeshaji wa jamii unaolenga kukuza maendeleo endelevu, kupunguza umaskini, kuimarisha usawa wa kijinsia, kuongeza ajira na ujasiriamali pamoja na kuboresha ustawi wa jamii kupitia elimu, mafunzo na uwezeshaji wa wananchi.
Mwongozo huu umeandaliwa ili kutoa maelekezo ya utekelezaji wa CBT katika maeneo ya majukumu, maadili, uongozi, utendaji kazi na usimamizi katika ngazi zote za COPO.
Empowering Communities, Transforming Lives
🌐 Website: https://tinyurl.com/copoafrica
© 2026 Community Plus Organization (COPO)
All Rights Reserved
“WEZESHA, UWEZESHWE”