EWE, BABA WA MBINGUNI
1.Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo
Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!
2.Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa.
3.Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawawape sasa Wawe mmoja vivyo
4.Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni.
5.Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli.
6.Siku za duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea.
“>
MAPYA NI MAPENZI HAYO
1.Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa.
2.Kila siku, Mapya pia Rehema, wema, na afya, Wokofu, na msamaha, Mawazo mema, furaha.
3.Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao, Mungu atatueleza Yatakayompendeza.
4.Mambo yetu ya dunia Mungu atayang’aria, Matata atageuza Yawe kwetu ya Baraka.
5.Yaliyo madogo, haya Mungu tukimfanyia, Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.
6.Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote: Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.
“>
NINA HAJA NAWE
1. Nina haja nawe Kila saa; Hawezi mwingine Kunifaa.
Yesu, nakuhitaji Vivyo kila saa! Niwezeshe, Mwokozi, Nakujia.
2. Nina haja nawe; Kaa nami, Na maonjo haya, Hayaumi.
3. Nina haja nawe; Kila hali, Maisha ni bure, Uli mbali.
4. Nina haja nawe, Nifundishe Na ahadi zako Zifikishe.
5. Nina haja nawe, Mweza yote, Ni wako kabisa Siku zote.
“>
KAA NAMI
1.Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.
2.Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.
3.Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe? Bwana, kaa name.
4.Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami.
5.Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami.
“>
NI TABIBU WA KARIBU
Mwimbaji mmojawapo aliyeuimba vizuri na katika upako wa kipekee wimbo huu wa Tabibu wa Karibu ni marehemu Angela Chibalonza.
Tafadhali fuatilia wimbo wa Tabibu wa Karibu na Tuimbe Pamoja:
NI Tabibu wa Karibu, Tabibu wa ajabu
Na rehema za daima; Ni dawa yake njema
Hatufai kuwa hai; Wala hatutumai
Ila yeye kweli ndiye; Atupumzishaye.
Kibwagizo
Dhambi pia na hatia;Ametuchukulia,
Twenendeni na amani; Hata kwake Mbinguni.
Kibwagizo
Huliona tamu jina,Jina Lake YESU.
Yuna sifa mwenye kufa, Asishindwe na Kufa.
Kibwagizo
Kila mume asimame, Sifa zake zivume
Wanawake na washike, Kusifu jina lake.
Kibwagizo
Na vijana wote tena, Wampendao sana
Waje kwake wawe wake, Kwa utumishi wake
Kibwagizo
NI SALAMA ROHONI MWANGU
1.Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.
2.Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.
3.Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu.
4.Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu.
“>
AKIFA YESU NIKAFA NAYE
1.Akifa Yesu nikafa naye Uzima upya huishi naye; Humtazama mpaka nje: Nyakati zote ni wake yeye.
Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.
2. Vita sipigi visivyo haki, Na Bwana wangu hapiganiki; Beramu yake haitwaliki, Napo po pote hila sitaki.
3. Sina mashaka, akawa mbali; Mizigo yote aihimili; Ananituliza Imanweli, Nyakati zote mimi husali.
4. Sina huzuni na mimi sidhii; Simwagi chozi, wala siguni; Sikuti afa, ila kitini Daima hunifikiri mimi.
5. Kila unyonge huusikia; Kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenye kuniokoa Nyakati zote hunijalia.
“>
MUNGU NI PENDO
1.Mungu ni pendo, apenda watu; Mungu ni pendo, anipenda Sikilizeni furaha yangu, Mungu ni pendo, anipenda.
2.Nilipotea katika dhambi, Nikawa mtumwa wa shetani.
3.Akaja Yesu kuniokoa, Yeye kanipa kuwa huru
4.Sababu hii namtumikia, Namsifu yeye siku zote.
MWOKOZI MOYONI MWANGU
1.Tangu siku hiyo aliponijia, Akae moyoni mwangu, Sina giza tena, ila mwanga pia Kwa Yesu mwokozi wangu.
Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu.
2.Sina haja tena, ya kutanga-tanga, Ndiye kiongozi wangu. Dhambi zangu zote zimeondolewa, Na Yesu, Mwanawe Mungu.
3.Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu. Hofu zangu na hamu zimeondoka, kwa kuwa ninaye Yesu.
4.Siogopi tena, nikiitwa kufa, Yu nami daima, Yesu. Mlango wa Mbinguni ni yeye pia, “Tapita humo kwa damu.”
5.Nitaketi na yeye huko milele, Nisifu Mwokozi wangu. Nina raha moyoni majira yote, Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.
“>
HATA NDIMI ELFU
1. Hata ndimi elfu elfu, Hazitoshi kweli Bwana Yesu kumsifu, Kwa zake fadhili.
2. Yesu, jina liwezalo Kufukuza hofu; Lanifurahisha hilo, Lanipa wokovu.
3. Jina hilo ni uzima; Ni afya amani; Laleta habari njema; Twalipiwa deni.
4. Yesu huvunja mapingu Ya dhambi moyoni; Msamaha, tena nguvu, Twapata rohoni.
5. Kwa sauti yake vile Wafu hufufuka Wakafurahi milele, Pasipo mashaka.
6. Ewe Yesu wangu Bwana, Uwezo nipewe, Kuhubiri kote sana, Wote wakujue.
“>
YESU UNIPENDAYE
1.Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni, Mwako maisha yangu; Nifiikishe mbinguni Wokoe moyo wangu.
2.Ngome nyingine sina; Nategemea kwako. Usinitupe Bwana , Nipe neema yako, Ninakuamania Mwenye kuniwezesha; Shari wanikingia, Vitani wanitosha.
3.Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; Nao waangukao Wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, Uongoze vipofu.
4.Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha Yapatikana kwako; Kwako Bwana naona Kisima cha uzima; Mwangu moyoni Bwana, Bubujika daima.
NIMEKOMBOLEWA NA YESU
1.Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake.
Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.
2.Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake.
3.Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu; Na sasa najifurahisha, Katika neema yake.
4.Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo.
“>
NAMWANDAMA BWANA
1.Namwndama Bwana kwa alilonena Njia yangu huning’azia; Nikimridhisha atanidumisha Taamini nitii pia.
Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.
2. Giza sina kwangu wala hata wingu Yeye mara huviondoa Woga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.
3. Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki Taamini nitii pia.
4. Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumpa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia.
5. Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda, nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia.
“>
YESU KWA IMANI
1.Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo.
2. Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu.
3. Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata.
4. Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo name Nami nikwandame Siku zote.
“>
NIONGOZE, BWANA MUNGU
1.Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, nguvu sina: Nishike mkononi; U mkate wa Mbinguni, nilishe siku zote.
2.Kijito cha maji mema, Kitokacho mwambani, Nguzo yako, moto, wingu, Yaongoza jangwani; Niokoe mwenye nguvu; Nguvu zangu na ngao.
3.Nikikaribia kufa, Sichi neno lolote, Wewe kifo umeshinda Zinawe nguvu zote, Tutaimba sifa zako, Kwako juu milele.