Mazungumzo.
Ni utanzu mojawapo wa fasihi simulizi .
Ni utaratibu wa kuongea baina ya pande mbili tofauti kuhusu mada mbalimbali zinazobadilikabadilika ambapo kwa kawaida wahusika wake huwa ni binadamu.
Sifa Za Mazungumzo
- Mada hughafilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine.
- Hahiitaji taaluma yoyote ya sanaa.
- Mandhari yake si rasmi bali mahali popote m.f njiani n.k
- Huwa na ucheshi mwingi.
Umuhimu wa Mazungumzo
- Huunganisha watu katika jamii
- Hutumiwa kama chombo cha kuburudisha katika jamii.
- Vilevile huelimisha kuhusu mambo fulani
- Pia huleta umoja na utangamano
- Hutumiwa kuonya dhidi ya matendo mabaya.
- Hutumiwa kupitisha wakati.
Vipera vya Mazungumzo.
- Malumbano ya utani.
- Ulumbi
- Soga
- Mawaitha
- Hotuba.