Yesu Ni Nani?

YESU NI NANI?

Miaka elfu nyingi ilizopita Mungu aliziumba mbingu na nchi, akaumba njua, mwezi na nyota, miti yote, maua na nyasi. Akaumba ndege wa angani, samaki na wanyama, lakini kilichokuwa kizuri katika kazi ya vyumbe vyote vya Mungu ilikuwa ni mtu.

Mungu aliumba mtu na alipoona kwamba huyu yuko peke yake, Mungu aliuumba mwanamke pia ili awrafiki na msaidizi wa mume. Na mwanamume akamuita Adamu na mwanamke akaitwa Hawa na numewe.

Shamba nzuri lililoitwa Edeni lilitayarishwa na Mungu kama kakao ya Adamu na Hawa. Hatujui ni muda gani waliishikwa furaha. Lakini twajua kwamba kwa muda walipomuheshimu Mungu bila ya kutenda dhambi, walikuwa na furaha.

Ndani ya shamba hili, Mungu aliweka miti miwili ya maana sana. Miti hii haikuwa ya Adamu na Hawa, mbali ilikuwa ya Mungu Mungu alitaka Adamu kama mwanamume kuitunza, lakini hakuruhusiwa kula matunda yao. Mti mmoja ulikuwa na maarifa ya kujua mema na mabaya. Na mwingine alikuwa mti wa uzima. Kula tunda la mti wa pili ulimaanisha kwamba mtu hangekufa daima.

Mungu hakutaka mtu ajue mabaya, hivyo, hakutaka watoto wake wale matunda ya mti huo. Ni kama vile hatutaki watoto wetu kutenda dhambi na kuhusika na mambo yaliyo mabaya duniani humu. Mungu hakutaka Adamu na Hawa kupoteza utamu wa maumbile yao. Maumbile ni usafi, uzuri na utakatifu.

Kulikuwa ni miaka mingi kabla ya Mungu kuumba ulimwengu mahali ambapo Mungu alikuwa ametayarisha huko mbinguni ambapo panaitwa MBINGUNI. Mungu alikuwa ametengeneza maelfu na maelfu ya viumbe vya mbinguni ambavyo vilimsifu na kumwabudu. Viumbe vya mbinguni hivi vinajulikana kwetu kama malaika. Kulikuwako na mpango maaluu kati ya majeshi haya. Nahodha wasaidizi kwao walikuwa malaika wakuu ambao waliitwa wakuu wa malaika.

Wakati mwingine wa miaka iliyopita, mmoja wa viongozi wa malaika ambaye jina lake aliitwa Lusifa alianza kujiona na kuasi. Upande wake alishinda mkubwa wa malaika na kwa pamoja walianza kupigania kiti cha enzi ambacho ni cha Mungu pekee. Matokeo yake ni kwamba Mungu aliadhibu Lusifa na malaika wake ambao waliasi kwa kuwatup nje watoke mbinguni. Mungu akatayarisha mahali pahukumu kwao. Mahali hapa pa hukumu ambao ni ziwa la moto panaitwa Jehanamu.

Kama matokeo ya kuanguka kwake Lusifa ambaye ni pepo, alimchukia Mungu na kutafuta nija ya "Kumlipa" kwa kujaribu kazi nzuri ya uumbaji wa Mungu. Shambani mwa Edeni akaja kwa mfano wa nyoka na kwa maarifa na ujanja wake akamdanganya Hawa ili ale tunda la mti wa maarifa. Hawa naye akampa hilo tunda Adamu ambaye peye pia alilia.

Mungu aliwaadhibu kwa kuwaamrisha waache shamba la Edeni. Alifanya hivi sababu alijua wangejaribwa kula tunda la mti wa uzima na wapate kuishi milele ndani ya dhambi zao. Na Mungu hangeweza kuwa na ushirika na huyo mtu ambaye aliimuumba kuwa na yeye mwenyewe.

Laana ya Mungu ilikuja kwa jamii ya kwanza sababu ya dhambi yao ya kutotii. Tangu hapo kizazi hicho watu wa ulimwengu huu tangu kale leo, wanazaliwa na tamaa ya kutenda dhambi. Hii dhambi ya kawaida yenyewe si muda mrefu baada ya mtoto kuweza kuzungumza na wakati mwingine hata kabla.

Huzuni ya Adamu na Hawa walikpofuk;uzwa na Mungu watoke katika makao yao mazuri ya Edeni, ilikuwa kubwa sana. Mungu aliwaahidi kwamba angewatumia mtoto mwanamume ambaye angeliwaokoa kutoka katika laana ya dhambi. Miaka elfu nyingi iliyopita hadi hii ilisemwa na kurudiwa kutoka kwa bab hadi mwana. Kizazi baada ya kizazi walingojea kuja kwa mwana ambaye angechukuwa dhambi zao na kuwafanya huru kutoka kwa hukumu ya dhambi. Kila wakati watu walitatizwa na kungoja, Mungu akatuma wajumbe wake, na manabii kuwahimiza wawe na imani na tumaini ili wangojee muda mfupi.

Nyakati za utawala wa kirumi duniani zaidi ya miaka elfu moja mia tisa iliyopita Mungu alitimiza ahadi yake. Mtoto mwanawe aliyeahidiwa, aliitwa Yesu, maana yake mwokozi. Mungu alikuwa amesema kuwa huyu mtoto ambaye angezaliwa kwa bikira Maria, alikuwa wa ahadi na ndiye aliyengojewa, mwokozi wa ulimwengu. Malaika alimwambia kwamba ingelikuwa kimiujiza mtoto kuzaliwa ambaye hana mzazi wa kiume. Maria alikuwa hajaolewa wakati wa kuzaliwa mtoto, au hakuwa na uhusiano na mume yeyote. Huyu hakuwa mtoto wa kawaida kwa vile alikiwa wa Mungu mwenyewe, yule aliyekuwa na Mungu tangu mwanzo wa dunia na aliyekusudia kuchukuwa mfano wa mwanadamu, na azaliwe kama mtoto.

Yesu alikaa maika thelathini na tatu katika ardhi ya Israel. Alionyesha watu upendo wa Mungu kwa kuwapenda wote. Aliponya wagonjwa, vipofu walifanywa kuona, vilema wakatembea, viziwi walisikia na bubu walinena. Alifukuza roho chafu kuwatoka wale waliokuwa wamepagawa nazo, aliwafufua wale walokuwa wamekufa na akafenya miujiza mingi. Watu walimpenda na wengi wakamwamini na kumfuata, lakini wakuu wa dini walikuwa na wivu kwa uwezo wake kwa watu na wakamvizia kumuua. Siku moja walimuamsha masaa ya asubuhi wakamleta mbele za makuhani na viongozi wa siasa na baada ya kesi na ushahidi usio wa kweli dhidi yake walimhukumu kifo kwa kumsulubisha. Ilikuwa ni desturi ya Kirumi kusulubisha wahalifu wabaya.

Walifurahia kwa ushindi wao mkuu, lakini kwa muda mrefu. Baada ya siku tatu baada ya kifo chake, Yesu Kristo mwokozi, alifufuka kutoka kwa wafu, akatoka ndani ya kaburi na kutokea kwa siku arobaini mbele ya rafiki zake na wanafunzi ambao baadaye walitoa habari za kufufuka kutoka kwa wafu. Yesu baada ya hayo alichkuliwa juu mbinguni, ambo yuko hata leo.

Kwa nini alikufa? Ilikuwa sababu hakuwa na nguvu ya kujiokoa? La, angelik;uwa ameita malaika kutoka mbinguni ili wamweke huru. Alikuwa mwana wa Mungu lakini alikufa kwa kusudi. Alikufa kwa kuumia kwa adhabu ya dhambi. Alihukumiwa na Mungu. baba yake mwenyewe, na hukumu tungelihukumiwa sisi. Alirudisha ushirika kati yetu na Mungu ambao dhambi ilivunja.

Hii siyo hekaya, inaweza kusikika kuwa geni kwako kama hukusikia mbeleni, lakini kwetu sisi tulioliamini, limekuwa mfariji wetu, furufa yetu na amani yetu. Ikiwa utaamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na ya kuwa alikufa kwa ajili yako, nawe pia utapokea msamaha wa dhambi zako na kupata uzima wa milele. Yesu atakuwa mwokozi wako. Anakupenda, alikufa kwa ajili yako. anataka umpenda na uishi naye na kuwaambia wengine habari hii ambayo nimekwisha kukuambia.

Kama utakataa na kugeuka utoke kwa upendo wa Mungu utahukumiwa. Hukumu yako itakuwa nini? Utahukumiwa katia ziwa la moto ambalo lilitayarishiwa shetani na malaika wake. Lakini ukiamini utaokolewa kutoka moto huu wa ajabu utakapokufa. "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili Kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele." Yohana 3:16.

Ikiwa baada ya kusoma hadithi ya uzima wa Yesu na kifo chake na ukiwa unataka kuwa mfuasi wake na kuwa mmoja wa jamii ya Mungu, inamisha kichwa chako sasa na uombe ombi hili fupi.

"Baba ulije mbinguni, naja kwako sasa, nakubali kuwa mwenye dhambi. Ninajua kuwa nimetenda dhambi. Siwezi kujibadilisha mwenyewe ila ni wewe kunibadilisha. Nakuomba unisaidie. Asante Yesu, kwa kufa kwa dhambi zangu. Asante kwe kunichukulia hukumu zangu. TAfadhali unisamehe sas. Tafadhali chukuwa dhambi zangu. Unifanye mtoto wa Mungu. Ninakukubali sasa kama mwokozi wangu. Nitakupenda, maishani mwangu mwote, nitakuishia na ikiwa lazima nitakufa na wewe. Badilisha maisha yangu na unifanye mweupe na mtakatifu kama wewe. Katika jina la Yesu naomba, Amina."

Acknowledgements

Swahili text courtesy of Engeltal Press, P.O. Box 447, Jasper, AR 72641, U.S.A.