Chromebook ni kompyuta ya kupakata inayotegemea Intaneti kwa utendaji mwingi na huhifadhi kiotomatiki kazi ya wanafunzi kutoka kwa programu nyingi kwa usalama katika Intaneti. Wakati mwanafunzi anapoingia kwenye Chromebook akitumia akaunti yake Google ya WPS, ni rahisi kupata kazi yake ya awali, kufikia Classrooms zilizo na mazoezi, kukutana walimu, na kumaliza mazoezi kwa kutumia programu na tovuti mbalimbali.
WPS Student Device Guide_Swahili 2022.pdf
Suluhu za Kawaida za Chromebook
Je, nifanye nini iwapo Chromebook yangu haiwaki?
Hakikisha Chromebook yako imechomekwa kwenye umeme. Unapaswa kuona taa ndogo karibu na eneo la kuchaji.Â
Bofya kitufe cha kuwasha/kuzima. Utakipata kwenye pembe ya juu kulia ya kibodi. Subiri sekunde 10 ili uone ikiwa hii itafanya kazi.
Ikiwa Chromebook bado haiwaki, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Usaidizi wa Teknolojia kwa maagizo zaidi au uwasilishe tiketi ya usaidizi.
Je, nifanye nini iwapo nimeshindwa kuunganisha na WiFi?
Hakikisha una mawimbi dhabiti ya WiFi. Unaweza kuhitaji kusogea karibu na chanzo cha WiFi (kisambaza data au mtandao pepe).
Hakikisha unatumia nenosiri sahihi kwa WiFi yako. Kuwa mwangalifu kwa herufi na nambari ambazo zinaweza kuonekana kama zinafanana 1 (moja), l (herufi ndogo ya L), na I (herufi kubwa ya i).
Ikiwa bado una tatizo, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Usaidizi wa Teknolojia kwa hatua zaidi au uwasilishe tiketi ya usaidizi.
Je, nifaye nini iwapo nimeshindwa kuingia katika Chromebook yangu?
Sababu ya kawaida ya tatizo hili ni kutokakana na makosa ya tahajia tu. Angalia tahajia yako kwa uangalifu na uzingatie herufi na nambari ambazo zinaweza kuonekana kama zinafanana kama vile 1 (moja), l (herufi ndogo L), na I (herufi kubwa ya i).
Ikiwa tahajia ni sahihi kabisa, unaweza kuomba nenosiri ili akaunti yako iwekwe upya. Tuma barua pepe na jina la mwanafunzi na nambari ya kitambulisho kwa mailadmin@worcesterschools.net na uombe upya nenosiri. Mara tu litakapowekwa upya, nenosiri litakuwa tarehe ya kuzaliwa ya mwanafunzi: MMDDYYYY.
Je, nifanye nini iwapo nimeshindwa kurekebisha tatizo la Chromebook yangu?
Kwa tatizo lolote ambalo umeshindwa kurekebisha kwa kutumia maelezo kwenye tovuti yetu, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Usaidizi wa Teknolojia.