Tahadhari za Jumla ili Kuhakikisha Utunzaji Unaofaa wa Kifaa cha Mkononi
Weka vyakula na kinywaji mbali na kifaa.
Kanda, nyaya, na vifaa vya kuhifadhi vinavyoweza kutolewa (hifadhi za USB) lazima viingizwe kwa uangalifu kwenye kifaa.
Vifaa havipaswi kutumiwa au kuhifadhiwa karibu na wanyama kipenzi.
Vifaa havipaswi kuwa katika mazingira yenye halijoto kali, kama vile kuachwa kwenye gari usiku mmoja wakati wa msimu wa baridi au siku yenye joto jingi.
Hakuna stika au maandishi/michoro inapaswa kuwekwa kwenye kifaa.
Vitu vizito (ikiwa ni pamoja na vitabu) havipaswi kuwekwa juu ya vifaa.
Kubeba Kifaa cha Mkononi
Inua au ubebe kifaa wakati tu kimefungwa salama; usiinue na usibebe kwa kushika skrini au wakati kifaa kiko wazi.
Utunzaji wa Skrini
Skrini inaweza kuharibika ikiwa inakabiliwa na vitu vizito, kushikwa kwa njia isiyofaa, na kumwagiwa viyeyusho vya usafishaji, na viovevu vingine. Skrini ni sehemu nyeti haswa kwa uharibifu unaotokana na mkazo mwingi.
Usihifadhi kifaa huku skrini ikiwa wazi.
Hakikisha hakuna kitu juu ya kibodi kabla ya kufunga kifuniko (kwa mfano kalamu, penseli).
Safisha skrini tu kwa kitambaa laini, kikavu, chenye nyuzi ndogo au kitambaa kisichosababisha umeme juu ya kifaa.
Lebo za Mali
Vifaa vyote na kanda zake za nishati zitawekwa alama ya lebo ya mali ya Worcester Public Schools. Lebo ya mali inaonyesha kuwa vifaa ni mali ya Worcester Public Schools.
Lebo za mali haziwezi kubadilishwa au kuharibiwa kwa njia yoyote.
Wanafunzi wanaweza kutozwa hadi gharama kamili ya kifaa kipya kwa kuharibu lebo ya mali wanaporudisha kifaa.
Hakikisha Chromebook yako imechajiwa kwa kuichomkea kwenye umeme. Unapaswa kuona taa karibu na eneo la kuchaji kwenye kompyuta.
Ifuatayo, fungua Chromebook na usubiri sekunde 10. Ikiwa hakuna kinachotokea, bonyeza kitufe cha kuwasha/kuzima kwenye kibodi.
Omba mtu mzima akusaidie kuwasiliana na mwalimu wako ili aweke upya nenosiri lako. Fuata maagizo ya mwalimu wako ili uingie tena.
AU Omba mtu mzima akusaidie kutuma ujumbe kwa mailadmin@worcesterschools.net ili uwajulishe kuwa akaunti yako haifanyi kazi. Watajibu ujumbe yakiwa pamoja na maelekezo.
AU Wasiliana na Fundi wa Teknolojia au Mkufunzi wa Teknolojia aliyeorodheshwa kwenye ukurasa huu.
Wilaya ina bima kwa uharibifu na umwagikiaji wa viowevu kwenye Chromebook. Tafadhali mjulishe mwalimu wako au mwalimu mkuu wako mara moja ikiwa Chromebook imeharibika ili iweze kurekebishwa. Itarekebishwa bila malipo kwako.
Wilaya HAINA bima ya wizi au upotezaji kwa hivyo tafadhali ilinde Chromebook na uiweke salama. Tenga chumba ndani ya nyumba yako ambapo kifaa kitarudishwa na kuchajiwa mwishoni mwa siku. Tazama ukurasa wa 8 kwa maelezo kuhusu wizi, upotezaji au jinsi ya ripoti uharibifu.