Ushirikiano wa pamoja uliotumika katika mchakato wa kuandaa onesho hili umejikita katika kuhusisha sauti mbalimbali ambazo kwa kawaida hazisikiki katika mazingira ya makumbusho au taaluma ya sayansi jamii kwa ujumla. Ushirikiano huu umejumuisha watafiti, Wazaramo, wataalamu wa makumbusho, wasanii, na wanafunzi ambao wameshirikiana kubuni, kufasiri, kupanga, au kutekeleza mradi huu. Mbinu hii ya sayansi shirikishi ni muhimili wa maarifa shirikishi yenye tija katika kuleta matokeo endelevu yatakayohimarisha Utamaduni wa Wazaramo ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Chakula changu kinatoka wapi, how the city eats.