Katika kabila ya WaSongola, wanaachanisha kundi ya watu kutoka juu ya bahari mpaka chini: Bisiulu, BaEnya, BaKuko, BaOmbo, BaBinja, and BinaIkese (Tazama Plan 2). Watu wanaoishi pembeni ya bahari ni walobaji, watu wanaoishi porini wanalima shamba na wanawinda wanyama. Walobaji na walimaji husaidiana kwa soko ya asili ya kubadilishana samaki na chakula.
Kati ya haya makundi ya watu, KiOmbo (C-69 katika uainishaji wa lugha za KiBantu), lugha ya BaOmbo kinafanana na lugha za BaMongo wanawoishi maghabiri wa bahari. Matamko ni mbalimbali kidogo kati ya makundi ya WaSongola. Bw. A.E.Meeussen, alitokaka Belge, akafika Maniema, kwa miaka wa 1950-1951kufanya utafiti wa lugha. Alikuwa na masikio mazuri sana na mdomo mwepesi wa kuweza kutamka kamili lugha mbaliimbali. MSongola moja wa Kailo alimwambiaka Bw. Meeussen ya kama lugha yake ni KiBinja. Kumbe, Bw. Meeussen aligeuza jina ya lugha kutoka KiSongola kwa KiBinja nord (D-24), kufananisha na KiZimba chenye kilianzaka kuitwa KiBinja sud tangu ile wakati.
Tazama Plan1
Tazama Plan 2