Ikiwa ungependa kuzungumza na mfanyakazi wa Worcester Public Schools kwa lugha nyingine isipokuwa Kiingereza, Wilaya ina wakalimani wa simu kwa zaidi ya lugha 240 ambao wanapatikana wakati wowote. Unapoipigia shule simu, mweleze mtu anayejibu simu kuwa unahitaji mkalimani. Atakuagiza usubiri kwa muda mfupi wakati anapotafuta mkalimani kwenye simu ili akusaidie. Ikiwa wakati wowote unahitaji kuzungumza na mwalimu fulani au mfanyakazi mwingine, unaweza pia kumtumia barua pepe ukimwomba akupigie simu na akiwa na mkalimani kwenye simu, au hata uombe kuratibu saa za kuwa na mkutano wa video na mwalimu pamoja na mkalimani.