Tunafurahia kuwajulisha kuwa WPS inaanzisha matumizi ya Remind WPS-nzima! Ikiwa huifahamu, Remind ni zana ya mawasiliano darasani inayorahisisha kuhusika kwako katika mafunzo ya mtoto wako. Remind hailipishwi na unaweza kuitumia kwa urahisi na utaweza kupokea na kutuma ujumbe katika kifaa chochote—hata ujumbe mfupi kwa simu yako!
Kama njia ya kuanzisha mpango huu, tutawaundia akaunti rasmi walimu, wazazi na wanafunzi wote katika WPS. Unaweza kupokea barua pepe au ujumbe wa simu kutoka Remind uliotumwa na shule au mwalimu wa mtoto wako. Kile unachohitajika kufanya ni kufuata hatua kwenye ujumbe ili umalize kuweka mipangilio ya akaunti yako.
Remind Cheat Sheet - Swahili.pdf
Mkutano wa video ni njia ya kukutana na kuzungumza na watu kupitia intaneti. Washiriki wanaweza kuona wenzao na kusikilizana na kutumia vipengele maalum kama vile kushiriki skrini. Programu mbili ambazo WPS hutumia ni Google Meet na Zoom. Kwa njia nyingi, programu hizi zinafanana, lakini maelezo kadhaa yanatofautiana. Hufai kuwa na wasiwasi kuhusu ni programu ipi unaweza kutumia kwa sababu programu sahihi itafunguliwa unapobofya kiungo cha mkutano.