The True Vine Ministries ni huduma ya kiinjilisti inayojengwa juu ya msingi wa Yohana 15:1 — “Mimi ndimi mzabibu wa kweli.” Lengo letu ni kumwinua Kristo kwa njia ya mafundisho, ibada, sanaa za kiroho, na kushirikisha ujumbe wa wokovu kupitia njia zote za kisasa.


Huduma hii ilianzishwa kwa maono ya kuwaleta watu karibu na Mzabibu wa kweli, huku tukitumia vipawa vya kiroho, sauti ya kweli ya neno la Mungu, na teknolojia kama chombo cha kuwafikia wengi duniani. Tunahudumia kupitia:

- Mafundisho ya Biblia ya kina

- Video na vipindi vya kiroho kwenye YouTube

- Maombi ya pamoja na mshikamano wa rohoni

- Mafunzo ya kiimani kwa kizazi kipya


The True Vine Ministries ni mahali pa ufunuo, uponyaji, na kukuwa kiroho. Karibu upate pumziko katika Kristo.