Ili kupata alama zako za wanafunzi katika Schoology utafungua akaunti yako ya maalum katika Schoology kama ilivyo katika tovuti nyingine yoyote au programu ya simu (kama vile Instagram, benki au programu zingine). GRPS haiwezi kuona, kudhibiti, au kuweka upya jina la mtumiaji au nenosiri lako utakapoweka mipangilio yake- maelezo haya ni ya faragha kwako na Schoology.
1. Wasiliana na mwalimu wa mwanafunzi wako, katibu au mkuu wa shule ili kupata “Parent Access Code”. Hii itakuwa nambari ya herufi 12 ambayo inaweza kuwa nambari au herufi kubwa au zote mbili MFANO: AB12-CD34-EF56
2. Unapopata namba ya ufikiaji wa mwanafunzi, ingia kwenye Schoology:
● katika kompyuta kwa kufungua kivinjari cha tovuti na kuelekea katika www.schoology.com
● Katika simu kwa kuelekea kwenye duka sahihi ya programu hapa chini na kupakua
KWENYE KOMPYUTA:
1. Unapokuwa katika www.schoology.com., bofya “Sign up”, kisha ubofye “parent”
2. Andika namba maalum ya ufikiaji wa mtoto wako katika sehemu ya “access code” na ubofye “continue”
UKITUMIA PROGRAMU YA SIMU YA SCHOOLOGY
1. Pakua programu kwenye duka la programu
2. Bonyeza Sign Up for Schoology katika sehemu ya chini.
3. Chagua Mzazi.
4. Weka namba ya ufikiaji uliyopewa na mwalimu wa mtoto wako kisha ubofye Continue
5. Weka jina lako la Kwanza na Mwisho, anwani ya barua pepe au jina la mtumiaji na nenosiri la akaunti yako.
6. Teua kisanduku ili ukubali Privacy Policy and Terms of Use ya Schoology.
7. Bonyeza Sajili ili ukamilishe.