Bofya settings (mipangilio)
Bofya Wi-Fi
Pata Mtandao wako wa Wi-Fi, na uubofye
Weka Nenosiri na uunganishe
Unganisha kanda ya umeme kwenye chanzo cha nishati
Pata eneo la kuchaji katika upande wa chini wa iPad
Chomeka iPad ndani
Bofya na ushikilie kitufe katika sehemu ya juu mpaka ishara ya Apple ionyeshe na iPad iwake.
Bofya na ushikilie mpaka upau wa kutelezesha uonekane. Telezesha ili uzime.
Ikiwa una mtandao pepe wa WPS, tafadhali angalia ukurasa wetu wa usanidi wa mtandao pepe.
Hakikisha una mawimbi thabiti ya WiFi. Unaweza kuhitaji kusogea karibu na chanzo cha WiFi (kisambaza data au mtandao pepe).
Hakikisha unatumia nenosiri sahihi kwa WiFi yako . Kuwa mwangalifu kwa herufi na nambari ambazo zinaweza kuonekana kama zinafanana kama vile 1 (moja), l (herufi ndogo ya L), na I (herufi kubwa ya i).
Ikiwa bado una tatizo, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Usaidizi wa Teknolojia kwa hatua zaidi au uwasilishe tiketi ya usaidizi.