Hapo tarehe 27 March 2020, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bi Dkt. Inmi Patterson alizindua ruzuku kwa wanabiashara na wakulima wanaofanya kazi ya kuboresha maisha ya Watanzania katika hafla iliyofanyika katika Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam. Inatarajiwa kuwa ruzuku hiyo itawanufaisha moja kwa moja zaidi ya watu milioni moja katika mikoa 16 humu nchini na itaboresha huduma na fursa katika sekta za maji na usafi wa mazingira, afya, elimu na maendeleo ya kiuchumi.