MADRASA YA MTANDAONI KWA WANAOANZA KUSOMA QUR’AN
Madrasa hii ni kwa ajili ya Waislamu wanaotaka kujifunza Qur’an, lakini wanakabiliwa na changamoto ya muda kutokana na kazi au ratiba zao za kila siku. Masomo yanaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia Google Meet, WhatsApp, na YouTube, yakilenga kutoa elimu ya Qur’an kwa njia rahisi, inayofikiwa na kila mwanafunzi popote alipo.
VIFAA NA MAHITAJI YA MWANAFUNZI
1. Smartphone au Tablet – Kwa kufuatilia madarasa.
2. Intaneti – Kuunganishwa na madarasa ya mtandaoni.
3. Google Meet – Kwa kuhudhuria masomo ya moja kwa moja (live).
4. WhatsApp – Kwa mawasiliano ya nyongeza na masomo ya ziada.
5. YouTube – Kwa masomo yaliyorekodiwa na marejeo.
6. Ada ya Mwezi: TZS 2,000.
7. Daftari na Peni – Kwa kuchukua maelezo na mazoezi.
8. Kitabu cha Wanaoanza au Msahafu – Kwa kujifunzia.
9. Ratiba Rasmi – Inayopangwa na mwalimu na kufuatwa na wanafunzi.
MASHARTI YA KUJIUNGA NA KUSHIRIKI MASOMO
1. Uislamu na Tabia Njema – Mwanafunzi lazima awe Muislamu mwenye tabia nzuri na maadili mema.
2. Kujaza Fomu ya Usajili – Malipo ya kujaza fomu ni TZS 1,500 (kwa mara ya kwanza).
3. Malipo ya Ada – Ada ya kila mwezi ni TZS 2,000 na inalipwa tarehe 26–28 kila mwezi kwa wanafunzi wanaoendelea.
4. Malipo ni Binafsi – Ada inahusiana na masomo ya mwanafunzi husika pekee.
5. Kufuata Maelekezo – Mwanafunzi lazima afuate maelekezo ya mwalimu kwa ukamilifu.
6. Hudhurio la Vipindi – Ni lazima kuhudhuria madarasa angalau mara 2 kwa wiki.
7. Kazi na Mazoezi – Mazoezi yote yanayopokelewa kutoka kwa mwalimu yafanywe kwa wakati unaofaa.
8. Taarifa za Udhuru – Taarifa za udhuru ziwasilishwe kwa mwalimu mapema.
9. Mtihani wa Kuhitimu – Wanafunzi wa Mustawa 01 watahitimu baada ya kufanya mtihani maalum.
10. Utovu wa Nidhamu – Hatua zifuatazo zitachukuliwa kwa mwanafunzi anayekiuka:
• Hatua ya 1: Nasaha zitatolewa kwa mwanafunzi mara ya kwanza.
• Hatua ya 2: Kusimamishwa masomo kwa mwezi mmoja iwapo hatorekebika.
• Hatua ya Mwisho: Kufutwa masomo ikiwa utovu wa nidhamu utaendelea.
YANAYORUHUSIWA KWA MWANAFUNZI
1. Kuuliza maswali kuhusu masomo yake wakati wowote.
2. Kutafuta ufafanuzi wa mambo ya kidini kulingana na masuala yanayomtatiza.
3. Kuomba ushauri wa kielimu au vitabu vya marejeo kwa msaada zaidi.
4. Kutoa mapendekezo ya utaratibu bora wa masomo kwa njia ya nidhamu.
5. Kukosoa kwa nidhamu jambo lolote analoona haliko sawa na kupendekeza njia bora.
6. Kuomba mawasiliano ya mwalimu moja kwa moja kwa dharura au msaada wa ziada.
MALIPO NA JINSI YA KULIPA
• Ada ya Kila Mwezi: TZS 2,000.
• Ada ya Kujaza Fomu ya Usajili: TZS 1,500 (mara moja tu).
• Malipo ya Awali (Jumla): TZS 3,500.
Tuma malipo yako kupitia TigoPesa:
• Namba ya Simu: 0659812626
• Jina la Mpokeaji: Rajabu Abdallah
MAZINGATIO MUHIMU
• Madarasa ya moja kwa moja yatafanyika kupitia Google Meet, kwa mujibu wa ratiba rasmi itakayopangwa na mwalimu.
• Masomo ya ziada, mawasiliano, na marejeo yatapatikana kupitia WhatsApp na YouTube.
• Zingatia ratiba na maelekezo ili kufanikisha malengo yako ya kujifunza Qur’an kwa njia rahisi na ya kisasa.
Jiunge sasa na uanze safari yako ya kielimu!
Allah akujaalie kheri na mafanikio!