PRIVACY POLICY YA MAFINGA CONNECT
Tarehe ya Mwisho Kuchapishwa: 02 Aprili 2026
Mafinga Connect ("sisi", "programu yetu") inathamini privacy yako. Sera hii ya faragha inaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako unapotumia programu yetu ya simu.
1. Taarifa Tunazokusanya
Tunakusanya taarifa mbalimbali ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wetu:
Taarifa za Wasifu:
Unapojisajili, tunakusanya jina lako, barua pepe (email), na picha ya wasifu (ikiwa utatumia Google Sign-In).
Maelezo ya Bidhaa na Huduma:
Tunakusanya taarifa unazoweka unapotangaza bidhaa, kazi, au huduma za ufundi, ikiwa ni pamoja na picha, bei, hali ya bidhaa (mpya au iliyotumika), na maelezo ya ziada.
Mawasiliano:
Namba ya simu unayoweka kwenye matangazo yako ili wateja waweze kukupata.
Mahali:
Taarifa za eneo (kama vile Mafinga Mjini) unazoweka mwenyewe ili kusaidiana na wateja kujua bidhaa inapatikana wapi.
2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako:
Tunatumia taarifa tunazokusanya kwa ajili ya:
Kuonyesha matangazo yako kwa watumiaji wengine wa programu.
Kukuunganisha wewe na wateja au waajiri .
Kuboresha utendaji wa programu na huduma zetu.
Kutuma arifa (push notifications) kuhusu bidhaa mpya au mabadiliko muhimu.
Kuzuia matumizi mabaya ya programu, kama vile picha zisizofaa au matangazo ya kitapeli.
3. Huduma za Pande wa Tatu (Third-Party Services)
Programu yetu inatumia huduma zifuatazo ambazo zinaweza kukusanya taarifa kulingana na sera zao:
Google Firebase: Kwa ajili ya kuhifadhi data na uthibitishaji wa watumiaji .
Cloudinary: Kwa ajili ya uhifadhi .
Google AdMob: Kwa ajili ya matangazo .
4. Usimamizi wa Maudhui na Ulinzi
Tuna mamlaka kamili ya kufuta maudhui yoyote yanayokiuka vigezo na masharti yetu, ikiwa ni pamoja na matangazo ya uongo. Tukio lolote la makusudi la kukiuka masharti ya utumiaji litapelekea kufutwa kwa akaunti ya mtumiaji husika mara moja.
5. Haki za Mtumiaji
Una haki ya:
Kufuta matangazo yako wakati wowote kupitia sehemu ya "Wasifu Wangu".
Kuacha kutumia programu na kuomba kufutwa kwa taarifa zako.
Kumbuka: Ukifuta chapisho lako, halitaonekana tena kwa wateja na utapoteza fursa ya kupata wateja kupitia chapisho hilo.
6. Usalama wa Data
Tunajitahidi kutumia mbinu bora za kiufundi kulinda taarifa zako.
7. Mabadiliko ya Sera Hii
Tunaweza kusasisha sera hii mara kwa mara. Tutakuarifu kuhusu mabadiliko yoyote kwa kuweka sera mpya hapa au kupitia taarifa ndani ya programu.
8. Wasiliana Nasi
Ikiwa una maswali au maoni kuhusu sera hii ya faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Email: [Arzeeaukaoa@gmail.com]
Simu: 0658203493
Kampuni: Arzeea Company LLC