ALICE OTIENO
Tulia Lyricsš§
Tulia, tulia aaah, tulia, tulia aaah, tulia, tulia aaah, tulia, tulia aaah
Tulia, tulia aaah, tulia, tulia aaah, tulia, tulia aaah, tulia
Nivigumu, anajua
Tumezoea kujitumainia
Lakini nguvu zetu
Haziwezi tosha
Vita vyetu, si vya Dunia
Nivigumu, anajua
Tumezoea kujitumainia
Lakini nguvu zetu
Haziwezi tosha
Vita vyetu, si vya Dunia
Ye hataki hela
Hataki mwenye cheo
Ni Wewe tu, kumuaminia
Atakuponya, atakulinda
Atakuonyesha ye astahili sifa
Moyo wangu tulia,
Usichoke tulia
Anafika tulia
Atakushika tulia
Moyo wangu tulia
Amani yake ipo sasa
Na yeye anaweza
ImaniĀ pazaĀ sauti
Scriptures š
Zaburi 46:1 - "Mungu ndiye kimbilio letu na nguvu yetu, msaada wetu sikuzote ukiwapo katika shida."
Zaburi 18:2 - "BWANA ndiye mwamba wangu, na boma langu, na mwokozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu."
Mathayo 11:28-30 - "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."
Wafilipi 4:6-7 - "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."
Kumtegemea Mungu badala ya mambo ya kidunia:
Methali 3:5-6 - "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako."
Zaburi 20:7 - "Hawa watumainio magari, na hawa farasi; sisi tutamkumbuka jina la BWANA, Mungu wetu."
Uwezo wa Mungu wa kuponya na kulinda:
Isaya 41:10 - "Usiogope; kwa maana mimi ni pamoja nawe; usisitahili; kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu; naam, nitakusaidia; naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu."
Zaburi 91:14-16 - "Kwa kuwa amenipenda mimi, nami nitamwokoa; nitamweka mahali pakuu, kwa kuwa amajua jina langu. Ataniita, nami nitamwitika; nitakuwa pamoja naye wakati wa dhiki; nitamwokoa, na kumtukuza. Nitamshibisha kwa siku nyingi, nami nitamwonyesha wokovu wangu."