Mambo ya kuombea

Mambo ya Kuombea katika Huduma

 

Sisi kama Timu ya Waandishi na Wahariri wa Vitabu vya Neno la Mungu. Tunaamini yakuwa Maombi yaweza kubadilisha mambo.Kwa nuru ya Mathayo 7:7 "Ombeni nanyi mtapewa..."Tunapenda kukushirikisha kuungana nasi katika maombi.

Ombea upatikanaji wa fedha za kuchapisha vitabu hivi ili kuwafikiwa watumishi wa Mungu wengine walioko vijijini ambao hawana Computer na mtandao wa intaneti.

 

Ombea upatikanaji wa Computer 2 kwa ajili ya Timu ya hapa Musoma.Kwa sasa wanafanya kazi zao kwa kuazima Computer na wakati mwingine kutumia gharama kubwa ya kulipa watu wengine ili waweze kuchapa.

 

Ombea kwa Makanisa mengi hapa Tanzania wataona umuhimu wa kuiunga Mkono huduma hii ya Maandiko na kuwatayari kutumia mali ghafi zao kusaidia huduma hii.

 

Ombea upatikanaji wa waandishi wengi walio na wito wa kufanya huduma hii ya uandishi ili ujumbe wa Habari njema za Bwana wetu Yesu Kristo uweze kuwafikia watu wengi!

Ombea upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kununua CD tupu ili kusambaza maandiko haya katika CDs pia kwa watu wengine kusoma Neno la Mungu.

Mungu akikugusa kusaidia na chochote, wasiliana na Mratibu wa huduma Yetu Mwj. Samuel Mpanilehi kwa anwani hii: smpanilehi@gmail.com