kuhusu Huduma
 
 

Huduma yetu ni kuandaa Vitabu vya Maelezo ya Biblia kwa Kiswahili rahisi kwa ajili ya Wachungaji, Walimu na Wanafunzi katika vyuo vya Biblia pamoja na Watu wa kawaida hususani wale ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria katika vyuo vya Biblia.

Vitabu vyetu hasa ni kwa ajili ya kumsaidia mtu wa kawaida kusoma Neno la Mungu. Si kwa ajili ya Biashara wala kwa ajili ya Wanatheologia kufanya utafiti, ingawa vyaweza kusaidia. Lakini lengo hasa ni kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa watu katika utamaduni wao.

Tunakaribisha Mkristo yoyote aliye na wito wa kuandika bila kujali elimu yake ili mradi awe ni Mkristo anayemkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yake. Na awe anayekubali kuwa Biblia pekee ndiyo kiongozi wa maisha ya Mkristo. Baada ya kuwa vitabu vimeandikwa, tunazo timu za Wahariri ambao ni lazima elimu yao ianze na Shahada ya kwanza katika Theologia na kuendelea. Hivyo kabla ya vitabu kuingia katika Tovuti Yetu, lazima kwanza vitabu vihakikiwe kama lugha kweli ni rahisi na tena theologia yake ni sahihi.

Unaweza ku-chapa ua kurudufisha vitabu hivi ili mradi maelezo ya haki ya kumiliki yawepo katika kitabu unacho chapa au kurudufisha.

Kama unahitaji kuchapisha kitabu kwa wachapaji nakala nyingi, tafadhari wasiliana nasi ili kupata kibali cha maandishi.

smpanilehi@gmail.com