Historia Fupi ya Huduma

Karibu katika Maelezo mafupi ya Huduma
 

Mwaka wa 2003 Mchungaji Martin alitembelea nchi ya Uganda. Na huko alikutana na ndugu Henry Kalule ambaye alikuwa ni katibu Mkuu wa Chama cha Biblia Nchini Uganda.

Martin alimwonyesha baadhi ya vitabu vilivyo andikwa katika Kiingereza rahi (easyenglish Bible Commentaries). Ndipo Ndg. Kalule alishauri kuwa ingewa bora kazi hiyo njema iwemo pia katika Lugha ya Kiswahili kwani ingekuwa baraka kubwa kwa Watumishi wa Mungu wa Afrika Mashariki ambapo Kwa sehemu kubwa Lugha ya Kiswahili inatumika.

Mwezi wa February 2004, Martin alimtembelea Samuel Mpanilehi huko Mwanza kwa mara ya Kwanza. samuel na Martin wamekuwa wakiwasiliana kwa njia ya barua paper na simu. Samuel alikuwa akipokea Vitabu vya maelezo ya Biblia kwa Kiingereza rahisi toka kwa Martin kwa muda mrefu. Moyo wa Samuel uliguswa kuweka vitabu hivi katika Lugha ya Kiswahili kwa ajili ya Watumishi wa Mungu wa hapa Africa.

Kwa mara ya kwanza Samuel aliandika kitabu cha Waraka wa 1 Timotheo kwa kiswahili rahisi.Kitabu ambacho kimekuwa baraka kwa Watumishi wa Mungu wengi hapa Tanzania na Africa kwa Ujumla.

Kwa sasa kuna timu mbalimbali za waandishi hapa Tanzania. kwa maelezo zaidi angalia kuhusu timu.

Mpaka sasa kuna timu zingine katika nchi mbalimbali wanaoandika Maelezo ya Biblia katika Lugha rahisi katika Lugha 19.

Mungu akubariki unaposoma vitabu vyetu na haditi za Biblia kwa Kiswahili rahisi.