Insha‎ > ‎

Insha za Kubuni

Insha za ubunifu ni insha ambazo mwanafunzi huhitaji kubuni maudhui, mazingira, wahusika, na kadhalika kulingana na swali analorejelea. Insha hizi zinaweza kuwa za methali, mdokezo ama insha zenye mada ambazo hazina mtindo rasmi.

Insha za Mdokezo

Hizi ni Insha za ubunifu ambazo mwanafunzi hupewa kifungu cha maneno kinachopaswa kujitokeza katika insha yake. Baadhi ya insha za aina hii huwa zimetangulizwa na mwanafunzi hutakiwa akamilishe na nyinginezo huwa na kimalizio.  Japo mwanafunzi ana uhuru wa kuiendeleza insha yake atakavyo, ni sharti ajifunge katika maudhui yanayojitokeza katika mdokezo aliopewa.  Kwa hivyo, kabla ya mwanafunzi kuiendeleza insha yake, ni sharti atambue maudhui yaliyokusudiwa na mtahini.

 Insha za Methali

Methali huwa na sehemu mbili na ni lazima insha ya methali izipe sehemu zote mbili uzito sawa. Kwa mfano. Mpanda ngazi hushuka, 

 Katika insha yako ni lazima utoe hoja za kutosha kuonyesha kwamba mhusika fulani kweli alipanda ngazi. Mwandishi pia anapaswa kutoa hoja za kutosha kuonyesha namna mhusika huyo aliposhuka. Kwa mara nyingi, wanafunzi huzingatia tu sehemu ya kwanza ya methali katika insha yote huku sehemu ya pili ikijitokeza katika aya ya mwisho pekee. Kumbuka kwamba ni muhimu kuelewa maana ya methali vizuri kabla ya kuchagua insha ya methali.

                    Insha zenye Mada

Hizi ni insha ambazo mwaandishi hutakiwa kuzungumzia mada fulani kwa kutoa hoja ama maelezo. Insha hizi hazimhitaji mtahiniwa kuanza kusimulia hadithi yake bali ni kurejelea mada aliyopewa. Mwandishi wa insha kama hii  anapaswa kuwa na hoja za kutosha kuhusu mada aliyopewa kabla ya kuanza kuiandika. Hoja zote zinapaswa kujitokeza katika masimulizi yenye mtiririko wala si kuorodhesha hoja, moja baada ya jingine.

 

Insha hizi huwa insha halisia na hivyo mwaandishi hawezi kupigia chuku au kutoa hoja zisizo kweli. Kwa mara nyingi insha hizi hurejelea maswala ibuka katika jamii k.v njaa, ukimwi, kilimo, ufisadi, ukabila, n.k

Comments