Fasihi Simulizi
Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha ambayo hupitishwa kutoka kizazi hadi kingine kwa njia ya mdomo (masimulizi). Kuna tanzu nne kuu za Fasihi Simulizi: .    Uchambuzi   Sifa za Fasihi Simulizi, Umuhimu wa Fasihi Simulizi na Mbinu za lugha katika Fasihi Simulizi
  • Hadithi    Hadithi au ngano ni aina ya sanaa katika fasihi simulizi ambayo husimulia visa kwa njia ya mdomo na hutumia lugha nathari. Soma aina mbalimbali za Ngano katika ukurasa huu.           
  • Nyimbo      Nyimbo ni sanaa ambayo hutoa ujumbe kwa njia ya kuimba. Nyimbo hutumia lugha teule, fupi na huimbwa kwa sauti maalam. Ingia hapa ili kusoma mengi kuhusu nyimbo katika fasihi simulizi. Katika utanzu huu wa nyimbo kuna pia Ushairi na Maghani        
  • Tungo Fupi   Tungo fupi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno au sentensi chache kupitisha ujumbe wake. Kuna aina kadhaa za tungo fupi ambazo zimeelezewa hapa.          
  • Maigizo Maigizo ni sanaa ambayo huwa na wahusika zaidi ya moja wanaojibizana moja kwa moja ukumbuni. Kwa mfano, katika mchezo wa kuigiza, watendaji huigiza maneno ya wahusika. Maigizo yanaweza kushirikisha aina nyingine za fasihi kama vile nyimbo na tungo fupi. Jifahamishe zaidi kuhusu utanzu huu wa maigizo kwa kufungua ukrasa huu.