Sauti za Kiswahili
_________________________________________________________________________________
a, b, ch, d, e, f, g, h, i, j, k, l, m, n, o, p, r, s, t, u, v, w, y, z
Irabu na Konsonanti

Irabu
 a, e, i, o, u
Irabu zinapotamkwa, hewa haizuiliwi katika ala za matamshi 
 Irabu Sehemu ya Ulimi Midomo
 e,i MbeleMidomo imetandaza
aKatikati; ulimi huinuka na kutandazaMidomo imetandaza
 o,u NyumaMidomo imevirigwa

Konsonanti
 b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w,  y,  z 
Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi ( ulimi na midomo)

Sauti za konsonanti:
Sauti ghuna - konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti
Sauti sighuna - 
konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti

Aina za konsonanti
  Midomo Midomo +
 Meno
 Meno + Ulimi Ufizi Kaakaa + ufizi Kaakaa gumu Kaakaa Laini Koo Aina ya Sauti
Vipasuo
p
b
  
t
d
  j
k
g
 sighuna
ghuna
Vikwamizo /
Vikwaruzo

f
v
th
dh
s
z
  shkh
gh
 hsighuna
ghuna
Kipasuo-kwamizo     ch   sighuna

Nazali / 
Ving'ong'o

 m
  
 n
  
ny
 
ng'
  
ghuna

Kitambaza
   
 l
    
ghuna

Kimadende
   
 r
    
ghuna
Viyeyusho / 
Nusu Irabu
      
y

 w
 
ghuna

Vipasuo 

( p,b,k,g,t,d )

Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla

Vipasuo sighuna (p, k, t ) - hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti
Vipasuo ghuna (b, g, d ) - hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti

/p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo katika meno.
/p/ -  papa, pepea, pipi, popo, pua
/b/ - baba, bebea, bibi, bobo, bubu

/t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi
/t/ - taa, tetea, titi, toto, tua
/d/ dada, doa, dua

/k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini
/k/ - kaka, koko, kuku
/g/ - gae, gege, gogo, gugu

Kipasuo-kwamizo: ( ch ) 

Pia huitwa kituo-kwamizo -  

Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa

/ch/ - chacha, chechea, choo


Ving'ong'o / Nazali ( m,n,ng',ny )

Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kuzuia hewa kupitia kinywani; hewa hupitia puani.

/m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani
/m/ - mama, umeme, mimi,

/n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani
/n/ - nana, nene, nini, nono, nunua

/ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu
/ny/ - nyanya, nyenyea, nyinyi, nyoa, nyunyu

/ng'/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini
 /ng'/ - ng'ang'a, ng'oa

Vikwamizo ( d  f,v,dh,th, s,z,sh,h,gh)

Pia Vikwaruzo
Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba

Vikwamizo sighuna (f,th,s,kh,h,sh) - hewa haitikisi nyuzi za sauti
Vikwamizo ghuna (v, dh,z,gh)  -  hewa hutikisa nyuzi za sauti 

/f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita
/f/ - faa, fee, fua
/v/ - vaa, vua

/s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu
/s/ - sasa, sisi
/z/  - zaa, zeze, zizi, zuzu

/dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu
/dh/ - dharau, dhani
/th/ - thubutu

/gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi
/dh/ - dharau, dhani
/th/ - thubutu

/h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu
/h/ - haha, hii, huu

Kitambaza l )

Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi

/l/ -  lala, lea, lilia, lo! lulu

Kimadende r )

Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi.

/r/ - rai, rarua,

Viyeyusho ( y,w )

Pia huitwa nusu-irabu

Hutamkwa kwa utaratibu kwa kuleta ala za matamshi karibu sana lakini kuachilia hewa bila kuikwaruza.

/w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi 

/w/ - wawa, wewe, 

/y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu

/y/ - yaya, yeye, Sauti = Herufi moja au zaidi
Silabi = Sauti moja au zaidi

Shada / mkazo ni kiwango cha nguvu zinazoambatanishwa na utamkaji wa sauti au silabi fulani. Soma mengi zaidi hapa.

 Mofimu = silabi moja au zaidi
Neno = Mofimu moja au zaidi


Mofimu
Mofimu ni sehemu ndogo zaidi ya neno, yenye maana fulani.Mofimu inaweza kuundwa kwa silabi moja au zaidi.  Soma kuhusu aina za mofimu (Mofimu Huru na Mofimu Tegemezi)


Ala za Kutamkia
 • Meno
 • Ulimi
 • Midomo
 • Pua
 • Chemba cha Pua
 • Ufizi
 • Kaakaa gumu
 • Kaakaa laini
 • Kimio
 • Chemba cha Kinywa
 • Ncha ya ulimi
 • Bapa la ulimi
 • Shina la Ulimi
 • Koromeo
 • Kidakatonge
 • Kongomeo
 • Nyuzi za Sauti
 • Koo
 • Njia ya Chakula
Comments