Lugha‎ > ‎

Ngeli

Ngeli za Kiswahili huainishwa kulingana na viambishi mbalimbali ambavyo nomino tofauti huchukua katika umoja na wingi. Katika ukurasa huu wa tovuti yetu, tutaangazia ngeli mbalimbali za kiswahili. Hili kusoma jinsi majina mbalimbali hubadilika katika Umoja na Wingi, angalia hapa.

Pia angalia Udogo na Ukubwa wa maneno mbalimbali.

Mukhtasari wa Ngeli
Majedwali yafuatayo yatakupatia picha nzuri jinsi maneno katika ngeli mbalimbali hupatanishwa kisarufi. Chini ya majedwali haya tumeelezea kila ngeli kwa kina, pamoja na mofano zaidi.

Ngeli

Mfano

Viashiria

Viashiria Visisitizi

karibu

mbali kidogo

mbali zaidi

karibu

mbali kidogo

mbali zaidi

a - wa

mtu
watu

huyu
hawa

huyo
hao

yule
wale

yuyu huyu
wawa hawa

yuyo huyo
ao hao

yule yule
wale wale

ki - vi

kiatu
viatu

hiki
hivi

hicho
hivyo

kile
vile

kiki hiki
vivi hivi

chicho hicho
vivyo hivyo

kile kile
vile vile

li - ya

embe
maembe

hili
haya

hilo
hayo

lile
yale

lili hili
yaya haya

lilo hilo
yayo hayo

lile lile
yale yale

ya - ya

maji
maji

haya
haya

hayo
hayo

yale
yale

yaya haya
yaya haya

yayo hayo
yayo hayo

yale yale
yale yale

i - zi

nyumba
nyumba

hii
hizi

hiyo
hizo

ile
zile

ii hii
zizi hizi

iyo hiyo
zizo hizo

ile ile
zile zile

u - zi

ukuta
kuta

huu
hizi

huo
hizo

ule
zile

uu huu
zizi hizi

uo huo
zizo hizo

ule ule
zile zile

u - i

mti
miti

huu
hii

huo
hiyo

ule
ile

uu huu
ii hii

uo huo
iyo hiyo

ule ule
ile ile

u - ya

 

huu
haya

huo
hayo

ule
yale

uu huu
yaya haya

uo huo
yayo hayo

ule ule
yale yale

u - u

unga
unga

huu
huu

huo
huo

ule
ule

uu huu
uu huu

uo huo
uo huo

ule ule
ule ule

ku - ku

mahali
mahali

huku
huku

huko
huko

kule
kule

kuku huku
kuku huku

kuko huko
kuko huko

kule kule
kule kule

pa - pa

mahali
mahali

hapa
hapa

hapo
hapo

pale
pale

papa hapa
papa hapa

papo hapo
papo hapo

pale pale
pale pale

mu - mu

shimoni
mashimoni

humu
humu

humo
humo

mle
mle

mumu humu
mumu humu

mumo humo
mumo humo

mle mle
mle mle
ngeli

A- Unganifu

o-rejeshi

-enye(we)

o-ote

-ingi(ne)

a - wa

wa
wa

ambaye

ambao

mwenyewe

wenyewe

yeyote

wowote

mwengine

wengine

ki - vi

cha
vya

ambacho

ambavyo

chenyewe

vyenyewe

chochote

vyovyote

kingine

vingine

li - ya

la
ya

ambalo

ambayo

lenyewe

yenyewe

lolote

yoyote

jingine

mengine

ya - ya

ya
ya

ambayo

ambayo

yenyewe

yenyewe

yoyote

yoyote

mengine

mengine

i - zi

ya
za

ambayo

ambazo

yenyewe

zenyewe

yoyote

zozote

nyingine

nyingine

u - zi

wa
za

ambao

ambazo

wenyewe

zenyewe

wowote

zozote

mwingine

nyingine

u - i

wa
ya

ambao

ambayo

wenyewe

yenyewe

wowote

yoyote

mwingine

nyingine

u - ya

 wa

ya

ambao

ambayo

wenyewe

yenyewe

wowote

yoyote

mwingine

mengine

u - u

wa

wa

ambao

ambao

wenyewe

wenyewe

wowote

wowote

mwingine

mwingine

ku - ku

kwa
kwa

ambako

ambako

kwenyewe

kwenyewe

kokote

kokote

kwengine

kwengine

pa - pa

pa
pa

ambapo

ambapo

penyewe

penyewe

popote

popote

pengine

pengine

mu - mu

mwa
mwa

ambamo

ambamo

menyewe

menyewe

momote

momote

mengine

mengineNgeli za Kiswahili
Ngeli ya A - WA
Ngeli hii hutumika kurejelea viumbe vilivyo hai (wanyama na watu). Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwa sauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi. Hata hivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti. 
Mifano:
mgonjwa - wagonjwa, mchungaji - wachungaji, mwizi - wezi, mtu - watu
mbuzi - mbuzi, kware - kware, nyati - nyati
kifaru - vifaru

Ngeli ya KI - VI
Ngeli ya KI - VI  hurejelea  vitu visivyo hai ambavyo ambavyo majina yao huanza kwa KI- au CH- (umoja) na VI- au VY- (wingi)
Mifano:
kijiko - vijiko, kikapu - vikapu, kioo, vioo
choo - vyoo, chumba - vyumba, chuma - vyuma, chungu - vyungu 
Ngeli ya LI - YA
Ngeli ya LI-YA husimamia nomino zenye miundo mbalimbali. Licha ya majina ya vitu visivyo hai, ngeli hii pia hutumika kwa majina yote katika hali ya ukubwa (yakiwemo ya watu au wanyama). Majina mengi huanza kwa JI- au J- kwa umoja na hubadilishwa kuanza na MA- au ME- kwa wingi. Kunayo majina mengine ambayo huanza kwa sauti nyingine kama vile /b/, /d/, /g/, /k/, /z/ n.k ambayo huwekwa kwa wingi kwa kuongeza kiungo MA-
Mifano:
jimbo - majimbo, jicho - macho, 
jiko - meko, jino - meno,  
tunda - matunda, ua - maua, umbo - maumbo, bati - mabati, shimo - mashimo
jitu - majitu, jisichana - majisichana

Ngeli ya U - I
Ngeli ya U - I huwakilisha nomino za vitu visivyo hai na ambavyo majina yake huanza kwa sauti M - (umoja)
Mifano:
mfupa - mifupa, mtambo - mitambo, mfuko - mifuko 

Ngeli ya U - ZI
Ngeli ya U - ZI hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi.
Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti U-
Mifano:
ufunguo - funguo, ubawa - bawa,  ukuta - ukuta,  upembe - pembe

Majina ya silabi mbili katika ngeli hii huongezwa sauti NY- ili kuyaweka katika wingi 
Mifano:
ua - nyua, uzi - nyuzi, uso - nyuso, uta - nyuta, wimbo - nyimbo

Ngeli ya I - ZI
Ngeli ya I - ZI hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). Aghalabu haya ni majina ya vitu ambayo huanza kwa sauti N, NG, NY, MB, n.k
Mifano:
nyumba - nyumba, nguo - nguo, mbegu - mbegu, nyasi - nyasi, nyama - nyama

Ngeli ya U - U
Ngeli ya U - U huwakilisha majina ya vitu yasiyokuwa na wingi na ambayo huanza kwa U- au M- Majina haya huchukua kiambishi kiwakilishi U- kwa umoja na pia wingi.
Mifano:
uji - uji, unga - unga, wimbi, wimbo
mtama - mtama, 

Ngeli ya YA - YA
Ngeli ya YA - YA huwakilisha nomino za wingi na nomino za dhahania ambazo nyingi kati yake huanza kwa MA-. Majina katika ngeli hii huchukua kiambishi YA- katika hali zote. 
Mifano:
maji - maji, maziwa - maziwa, mafuta - mafuta, 

Ngeli ya Mahali PO - KU - MU
Ngeli ya PO hurejelea mahali maalum, padogo au palipo wazi.

Ngeli ya KU hurejelea mahali fulani kwa ujumla au eneo fulani. 

Ngeli ya MU - hutumika kurejelea mahali ndani ya kitu kingine. kama vile ndani ya nyumba, shimo n.k

Ngeli za mahali hubaki vivyo hivyo katika umoja na wingi

Soma kuhusu umoja na wingi wa majina katika ngeli mbalimbali katika ukrasa huu.

Comments