UTANGULIZI:
Kikuwa kilianzishwa mwaka 1990 kikiwa na jina la Mama Mluge youth and children group na kusajiliwa chini ya Baraza la sanaa Tanzania, Basata. Mwaka 2001 kikundi kimeongeza shughuli zake na kubadilika kuwa kituo cha watoto na kusajiliwa kama Shirika lisilo la kiserikali. SHUGHULI ZA KITUO Kuwajumuisha, kuwastawisha na kuwaendeleza watoto kiafya, kuimarisha na kujenga msingi bora wa maisha yao ya baadaye. Kuunganisha na kulmarisha uhusiano bora, kati ya watoto wote bila kujali rangi, dini, utaifa, umri, hali ya kimaisha na tofauti walizonazo kimaisha. Kukuza haki na kudumisha upendo kwa maisha yao ya baadaye. Kutetea haki na kudumisha upendo kwa watoto. Kuelimisha Wazazi, walezi na taifa kwa ujumla juu ya umuhimu wa haki za watoto na maendeleo yao. Kuwasaidia kielimu na kimaisha watoto waliokosa fursa kutokana na matizo ya kimaisha, familia na yatima hasa watoto na mitaani. MATARAJIO Kuanzisha kituo cha watoto ambacho kitakuwa na sehemu za burudani, elimu, kumbukumbu, mspumziko, mahali pa kukutania watoto, michezo na maonyesho ya kazi za mikono za watoto. UANACHAMA Wanachama wa kituo ni wazi kwa watoto wote wenye matatizo, bila kulazimishwa wanaruhusiwa kujinga na kupokea huduma wanazostahili kama haki zao na Kwa mtu yeyote aliye zaidi ya miaka 18 anayependa kufanya kazi na kuwasaidia watoto na kutambua umuhimu wa misaada wake kwa maisha ya baadaye ya watoto. |

